USIKU WA MAYENU KUZINDULIWA MZALENDO PUB LEO

WAKALI wa disko Fleva Nite linalopigwa kila Jumamosi katika Ukumbi wa Mzalendo Pub, leo wanatarajiwa kuzindua Usiku wa Mayenu, utakaokuwa ukifanyika kila Ijumaa katika ukumbi huo Mzalendo.

Msemaji wa Fleva Nite, Boniventure Kilosa ‘Dj Venture’ (PICHANI)alisema usiku huo wa mayenu utakuwa ukipigwa nyimbo mbalimbali za Kiafrika za mtindo huo wa mayenu.
“Tumeanza kupiga disko hilo maalumu kwa ajili ya mayenu Ijumaa iliyopita na mambo yalikuwa mazuri, wiki hii ya uzinduzi itakuwa bab, mashabiki waje waone kutakuwa na mambo mbalimbali ya kuburudisha,” alisema Venture.
Katika uzinduzi huo kutakuwa na wanamitindo mbalimbali kwa ajili ya kusindikiza na kutoa burudani kwa mashabiki watakaohudhiria hapo kesho.
Wanamitindo hao ambao watapamba uzinduzi huo wa usiku wa mayenu ni Rihama De Prada Burhan, Ally Dax, Angel na Lucky.
Disko hilo la ngoma za mayenu litashushwa na Madj wakali kama Makay Kilosa ‘Dj Makay’, Oscar Urio ‘Dj Oscar’, Dj Venture na Boniface Kilosa ‘Dj Bon Love’.
WAKALI wa disko Fleva Nite linalopigwa kila Jumamosi katika Ukumbi wa Mzalendo Pub, leo wanatarajiwa kuzindua Usiku wa Mayenu, utakaokuwa ukifanyika kila Ijumaa katika ukumbi huo Mzalendo.

Akizungumza na Papaso la Burudani msemaji wa Fleva Nite, Boniventure Kilosa ‘Dj Venture’ alisema usiku huo wa mayenu utakuwa ukipigwa nyimbo mbalimbali za Kiafrika za mtindo huo wa mayenu.

Comments