USHINDI WA 5-0 WALIEVYA YANGA


USHINDI wa mabao 5-0 uliowapata mabingwa watetezi wa ligi kuu bara Yanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga juzi, umewafanya wasahau matatizo yao ya kusuasua katika ligi hiyo.

Yanga ilipata ushindi huo jumatano iliyopita wakati ikiwa imekwenda ufukweni ili kuwawejengea stamina wachezaji wake na hivyo kuweza kufanya vema.
Baada ya kushinda mechi hiyo, Yanga iliamua kuwapa mapumziko mafupi wachezaji wake huku kocha wao mkuu, Mganda Sam Timbe akitimikia kwao kwa ajili ya kusalimia familia.
Kinachoonekana ni kwamba, ushindi huo umewafanya wasahau kwamba wanahitajika kuendelea kujifua ili kuwafanya wachezaji wao waweze kuhimili mikikimiki ya ligi hiyo.
Hadi sasa Yanga inashika nafasi ya nne katika msimamo huo ikiwa na pointi 12 katika mechi nane ilizocheza, imeshinda mechi 2, imetoka sare nne na kufungwa mechi mbili, wakati mahasimu wao Simba, wanaongoza kwa kuwa na pointi 18, wakifuatiwa na Azam yenye pointi 15.

Comments