TWIGA STARS KUANZA NA NAMIBIA CAN

TIMU ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars itaanza kampeni yake ya kuwania ya kufuzu kucheza fainali za Afrika katika fainali zitakazofanyika mwakani ambapo itaanza mzunguko wa awali kwa kukipiga na Namibia.

 Twiga, itaanza mzunguko huo kwa kucheza ugenini kati ya Januari 13, 14 na 15 mwakani, kabla ya kurudiana kati ya Januari 25, 26 na 27.
Endapo itafanikiwa kuitoa Namibia itacheza na mshindi kati ya Ethiopia utakaofanyika kati ya Mei 25, 26 na 27 na mchezo wa marudiano utafanyika kati ya Juni 15, 16 na 17 mwakani.
Katika mzunguko wa kwanza Tanzania imepangwa na timu Guinea, Ivory Coast, Msumbiji, Mali, Ghana na Algeria.
Aidha, timu za Afrika Kusini, Cameroon, Equatorial Guinea na Nigeria zimefuzu moja kwa moja mashindano hayo baada ya kushika nafasi za juu katika viwango vya soka.
Tanzania kama itafuzu kucheza michuano hiyo itakuwa ni mara ya pili baada ya kucheza fainali hizo mwaka jana zilizofanyika nchini Afrika Kusini.

Comments