TIMU YA 94KJ YAANIKA KIKOSI CHAKE

Wakati ligi kuu soka daraja la kwanza ikitarajia kuanza oktoba kumi na tano mwezi wa kumi mwaka huu timu ya soka ya 94 kj imetangaza kikosi chake chenye wachezaji ishirini na saba chini ya kocha mkuu mwinyimadi tambaza ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha kukuza viapaji kwa watoto chini ya miaka kumi na saba kidiyosa.

Tambaza amesema kwa sasa timu yake imekamilika vya kutosha na wanasuburi ligi kuanza ameongeza kuwa wachezaji waliosajiriwa kwenye timu hiyo wametimiza vigezo vyote vya soka na kusisitiza kuwa wachezaji ambao wameachwa ni kutokana na kushindwa kutimiza vigezo husika pamoja na kushuka kwa viwango katika eneo zima la ufundi wachezaji waliosajiriwa na timu hiyo ni
Ameir selemani Haji, kasuguri wilboard mwocha, Emanuel Anyelwise Kyomo,Mfaume said mfaume,fransisc Ubald Mjuni, Anthone Christopher silanda ,Edward Henry peter,Julius Rchard Mbaga,Osmund Anthony Banda,Abnel Omollo Mourice,juma mbaruk juma ,Said Asaa said,Katina shija Katina na kalist joseph mbonde wachezaji hao kumi na nne ndio walio kuwemo katika kikosi cha mwaka jana .
Katika wachezaji ishirini na saba ambao wanatimiza idadi ya wachezaji kwenye timu hiyo wachezaji kumi na tatu ni wapya kwa maana hawakuwahi kuchezea timu hiyo maishani mwao ambao kumi na tatu kati yao ni huru ukiacha mchezaji Nassoro khamis Makoba (Red coast) wachezaji walosajiriwa kwa usajiri huru ni Hamis shaban Claudio, Evance George Kachegwa ,Haruna athumani Kilundumya, Erick Leopod Mpunga ,Mohamed Maketem Abdalah , Abdalah Hasan Mbonde,joseph joseph mhagama,Murusari Zukheri Selemani,Simon Joel shadrack ,ally abdalah ally,Josephat Josephat Mabunda, na Daniel Charles Mecha.


Aidha timu hiyo imeacha jumla ya wachezaji kumi na tano ambao ally Abdalah Chitanda, Hafidh mwalimu, yavan andrea samaje, juma Rashid shaibu, samsoni jonathan yonazani, Bedastus Hosea Mwasambaili, Thomas Lusajo Mwakasagule, Shomari Abadalaah mbonde, Emanuel Mathayo China, Ibrahim Khamis Ame, Mohamed Othman Khamis ,Adamu said Adamu, Abeid said Ding’oko, Gondwin Samwel Sinda,na Abdul ismail Nayopa.


Wakati timu hiyo jeshi ikiwa inaendelea na mazoezi katika uwanja vinyago mwenge ipo kundi c pamoja na timu za samaria ya iringa, Rhino rangers ya tabora, polisi tabora tabaora, polisi morogoro na arusha football club ya Arusha .

Comments