TFF YAMCHINJIA BAHARINI MICHAEL WAMBURA



KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imemuengua kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya Mwenyekiti ya Chama cha soka Mkoani Mara (FAM), Michael Wambura kwa kukosa uadilifu wa kiuongozi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya TFF, Deogratius Lyato hatua za kumuengua Wambura na wagombea wengine wawili katika kinyang’anyiro hicho ziliamuliwa baada ya kikao cha kamati hiyo kilichoketi Oktoba 23 na 24.
Lyato alisema kamati kabla ya uamuzi huo ilipitia na kugundua kwamba pingamizi lililopitishwa na Titus Osoro dhidi ya Wambura kwamba lilikosa sifa ya kuwa rufaa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF katika ibara ya 11 (2) na (3).
Lyato alisema kwa mujibu wa Katiba ya TFF ibara ya 49 (1), Katiba ya FAM, Ibara ya 47 na kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF ibara ya 26 (2) ilimhoji Wambura kuhusu taarifa za kufungua kesi ya madai namba 100 ya mwaka 2010 kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam dhidi ya Mwenyekiti wa Simba kinyume na katiba ya Simba.
Alisema Wambura alivunja katiba ya Simba ibara ya 11 (2)b, amevunja katiba ya FAM ibara ya 12 (2)e, alikiuka katiba ya TFF ibara ya 12 (1) (d) na 12 (2) (e) na ya FIFA ibara ya 64 (2).
Lyato alisema Wambura pia alikiuka suala lingine la uadilifu kwamba amekuwa akitoa lugha ambazo si za kimichezo kwa kuziita Kamati za uchaguzi za TFF kuwa ni ‘Kangaroo Coarts’ ambako aameitaka sekretarieti ya TFF kuchukua hatua dhidi ya mwanamichezo huyo.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHOctober 27, 2011 at 4:53 AM

    UADILIFU HAUSOMEWI!UNAZALIWA NAO.MICHAEL RUDI ZAKO KWENYE CRICKET TU NDUGU YANGU,SOKA TENA SAHAU BROTHER!!

    ReplyDelete

Post a Comment