T- KWENDA KUFANYA MAMBO MTWARA OKTOBA 29 NA 30

KUNDi jipya la muziki wa taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ama ‘Real Madrid’ linatarajia kuanza kufanya maonyesho mawili katika mkoa wa mtwara.

Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini, alisema jana kuwa kuwa mara tu baada ya uzinduzi wa kundi hilo unaotarajia kufanyika Oktoba 28, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, kundi hilo tayari linamwaliko wa Oktoba 29 na 30, Mkoani Mtwara.
Alisema kuwa mara tu baada ya kumaliza onyesho la uzinduzi huo, wasanii wataondoka jijini usiku huo huona kuanza safari ya kuelekea Mtwara ambako watafanya maonyesho mawili.
“Onyesho la kwanza la oktoba 29, linatarajia kufanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Makonde Beach Club, na onyesho la pili litafanyika Oktoba 30 Nachingwea,”Alisema
Salmini alisema kuwa kabla ya kufanya onyesho la pili wasanii wa kundi hilo watatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa huo husasan wodi ya wazazi na watoto, ambapo watatoa msaada wa kitanda cha kuzalia katika hospitali hiyo pamoja na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto waliolazwa katika hospitali hiyo.
Aidha katika uzinduzi wa kundi hilo unaotarajia kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, bendi za Mapacha Watatu na Msondo Ngoma zitakuwa bega kwa bega katika kutoa burudani za kusindikiza na kulipa sapoti kundi hilo.
Albamu ya kwanza ya kundi hilo imebebwa na wimbo wa Bi Mwanahawa Ally, uitwao Aliyeniumba Hajanikosea, ambapo pia itakuwa na nyimbo nyingine kali zilizoanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio, zikiwemo Unavyojidhani Hufanani (Jokha Kassim), Mchimba Kaburi Sasa Zamu yake Imefkuwa (Mrisho Rajab), Riziki Shotcut ambao umeimbwa na Aisha Masanja.

Comments