SIMBA, YANGA ZATEGANA DAR ES SALAAM


MAHASIMU wa jadi nchini Simba na Yanga wameonekana kutegana katika maandalizi ya mechi yao ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajiwa kupigwa jumamosi kwenye dimba la Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kutogana huko kinatokana na kila timu kuendelea kubaki katika kambi yake ya kawaida tofauti na ilivyozoeleka pindi timu hizo zinapokaribia kukwaana kutoka nje ya jiji kwa ajili ya kusaka ubani.
Yanga ambayo imezoea kwenda kupiga kambi Kisiwani Mafia ama Bagamoyo ilikuwa na mpango wa kwenda Msumbiji jana kabla ya kufuta mpango huo na kuendelea kubaki makao makuu ya klabu hiyo MItaa ya Jangwani na Twiga, huku Simba nayo ikiendelea kupiga kambi yake ya muda mrefu katika hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Comments