SIMBA YAIFUNIKA YANGA STARS

KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya  Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na mchezo wa mwisho wa Kundi D, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani, chini ya kocha Mdenmark, Jan Borge Poulsen kimetawaliwa na wachezaji wa Simba SC.
Hiyo inafuatia Simba kuwa na wachezaji watano katika kikosi hicho huku Yanga ikibaki na wachezaji  wawili tu kati ya watatu waliokuwemo baada ya jana kuumia kwa nahodha wa Stars ambaye pia ni nahodha wa  Yanga, Shadrack Nsajigwa.
Kutokana na kuumia kwa Nsajigwa, nafasi yake imechukuliwa na Nasoro Said ‘Cholo’ , ambaye anaungana na Juma kaseja, Juma Nyoso, Juma Jabu na Victor Costa na kutimiza idadi ya wachezaji watano, huku Yanga ikibaki na kipa Shaban Kado na Nurdin Balari.
Azam nayo ina wachezaji watano kwenye kikosi hicho sawa na Simba ambao ni John Bocco, Ramadhan Chombo, Jabir Aziz, Aggrey Morris na Mrisho Ngasa, ingawa Wekundu wa Msimbazi wanakuwa mchango mkubwa zaidi kwenye kikosi hicho kutokana na wachezaji wa zamani ambao sasa wanacheza nje, kama Mbwana Samatta, Athumani Machuppa, Danny Mrwanda na Henry Jospeh. Lakini pia, viungo Jabir Aziz na Ramadhan Chombo, miaka miwili iliyopita walikuwa wachezaji wa Simba SC.
Akizungumzia suala la Nsajigwa, Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema kwamba beki huyo ameumia nyonga (groin) kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Karume,  Dar es Salaam.
Alisema kwa mujibu wa daktari wa Taifa Stars, Dk. Mwanandi Mwankemwa, maumivu hayo yatamweka Nsajigwa nje ya uwanja kwa kati ya wiki mbili hadi nne.
 “Kutokana na ushauri wa daktari, Kocha wa Stars, Jan Poulsen amemuondoa kwenye kikosi hicho ambacho kitasafiri Oktoba 6 mwaka huu kwenda  Casablanca , Morocco  kwa ajili ya mechi dhidi ya  Morocco  itakayochezwa Oktoba 9

Comments