SIMBA WALEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

SIMBA SC leo wamezidi kupasua mawimbi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 2-0 na kufikisha pointi 27 baada ya kucheza 11 za ligi hiyo. Shukrani kwao kiungo Jerry Evans Santo kutoka Kenya na mshambuliaji Felix Mumba Sunzu kutoka Zambia kwa mabao yao, ambayo yamezidi kuongeza matumaini ya ubingwa msimu huu. Santo alifunga bao hilo dakika ya 18, kwa kichwa akiunganisha krosi ya Uhuru Suleiman ‘Robinho’ na lilidumu hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza. Sunzu aliifungia Simba bao la kuhitimisha ushindi dakika ya kwanza tu ya kipindi cha pili, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’ na kumtungua kipa kipa ‘emolo’ Amani Simba.
Kwa ushindi huo, Simba imezidi kujikita kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 27 baada ya kushuka dimbani mara 11, ambapo hadi sasa haijapoteza mechi hata moja, huku ikilazimishwa sare tatu.

Comments