SIMBA, RUVU SHOOTING ZAINGIZA MIL.14

Mechi namba 66 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa Oktoba 19 mwaka huu Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam imeingiza sh. 14,755,000.

Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 2,794 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000 kwa mzunguko na sh. 10,000 kwa VIP. Waliokata tiketi za VIP walikuwa 157.

Baada ya kuondoa gharama za mchezo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,180,763 kila timu ilipata sh. 3,172,271.19. Mgawo mwingine ulikwenda kwa uwanja (sh. 1,057,423.70), TFF (sh. 1,057,423.70), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 528,711.86), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 422,969.49) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 105,742.37).

Comments