SIMBA KUIVAA LYON KESHO BILA MAFTAH, COSTA

WEKUNDU wa  Msimbazi Simba kesho watashuka kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kumenyana na African Lyon , huku ikiwakosa wachezaji wake mahiri, Amir Maftah,Victor Costa,Salum Machaku na Mwinyi Kazimoto
Hata hivyo, msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba wachezaji wengine wapo katika hali nzuri wanaendelea kujinoa katika kambi ya timu hiyo iliyopigwa kwenye hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam.


Lyon , kupitia kwa msemaji wake, Sheraly Ally,  alisema wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya mchezo huo ingawa wana wachezaji majeruhi watatu ambao ni Adam Kingwande anayesumbuliwa na nyama za paja, Benedictor Jacob anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu na Johannes Kagwa anayesumbuliwa na kidole cha mguu.
Ally alisema pamoja na kwamba Simba ni timu nzuri na wao wamejiandaa kuifunga kutokana na mafunzo aliyoyatoa kocha Mkuu Jumanne Chale.

Comments