SIMBA JUUUUUUUUUUUUUUUUU

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba leo wamerudi tena kwenye kilele cha ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kuichabanga African Lyon kwa mabao 4-0 katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar  es Salaam.
Mabao ya Simba yalipachikwa na Emmanuel Okwi aliyepachika mawili, Felix Sunzu na Shomari Kapombe ambao kila mmoja alifunga bao moja moja.
Kwa matokeo hayo, Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 21, ikifuatiwa na JKT Oljoro yenye pointi 19, huku Azam ikiwa ya tatu kwa pointi 18 na Yanga inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 15.

Comments