SERIKALI YAKATAA MAOMBI YA HIFADHI KWA WACHEZAJI WA RED SEA

SERIKALI imekataa maombi ya wachezaji 13 wa Timu ya Mpira wa miguu ya Red Sea ya Eritrea, waliokuwa wameomba kupewa hifadhi ya ukimbizi hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani Isaac Nantanga, maombi ya wachezaji hao hadi sasa yapo chini ya uagalizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi duniani (UNHCR).
Alisema kuwa, maombi hayo yamekataliwa kutokana na kukosa sifa za kupata hifadhi ya ukimbizi, na moja ya sifa hizo ni pamoja na kutoa ushahidi usio na mashaka wa kukimbia mateso au hali inayotishia maisha mwombaji.

Comments