POULSEN KUJA NA DOZI ZA CHAD KESHO

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’,Jan Poulsen, anatarajiwa kutua kesho akitokea mapumzikoni kwao, tayari kuanza maandalizi ya mechi ya kufuzu makundi ya Kombe la Dunia 2014, dhidi ya Chad.

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema Poulsen anatarajiwa kutua kesho ili kuweza  kukiandaa kikosi chake mapema kwa ajili ya mechi hiyo ambayo imepangwa kupigwa Novemba 11 jijini Djamena, kabla ya kurudiana siku nne baadaye jijini.

Comments