NIMEREJEA YANGA KWA MAPENZI YANGU-MANJI

MFADHILI wa Yanga, Yusuf Mehboob Manji amesema kurejea kwake kuifadhili klabu hiyo hiyo hakutokani na shinikizo mlolote bali ni mapenzi yake ya dhati aliyonayo kwa klabu hiyo.

Manji aliyerejea jana kutoka Marekani alisema amepokea maombi ya viongozi wa Yanga waliomuomba kurejea kuifadhili klabu hiyo ili kuiwezesha ipate mafanikio katika mashindano inayoshiriki ikiwemo Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

Moja ya mikakati mipya atakayoanza nayo ni kuhakikisha wanawafunga mahasimu wao Simba katika mechi yao ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara itakayopigwa, Oktoba 29 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Comments