NADIR CANNAVARO NA STAKI NATAKA STARS

BEKI wa timu ya Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' almanusura jana achafue hali ya hewa baada ya kusigana kimtindo na viongozi wa timu yake baada ya kudaiwa kugoma kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kinachotarajiwa kukwaana na Morocco Jumapili hii.
Inadaiwa kuwa, baada ya kuumia kwa beki wa Stars Victor Costa, kocha mkuu wa Stars Jan Poulsen alimwita Cannavaro kwa ajili ya kuziba pengo hilo, hata hivyo Cannavaro hakupendezwa na hali hiyo.
MMoja ya watu wa karibu wa Cannavaro alisema kuwa beki huyo hakupendwa kuitwa kundini kwa ajili ya kuziba pengo la mtu kwani hali hiyo inaonyesha kuwa hana thamani yoyote ndani ya kikosi hicho.
"Anachodai Cannavaro ni kwanini kocha asimuite Poulsen tangu awali alipoita kikosi hicho,?Alihoji mtoa habari huyo.
Aidha, kufuatia 'mgomo baridi huo' ilibidi uongozi wa Yanga uingilie kati na kumsihi mchezaji huyo arudi nyuma na kuitia mwito wa Poulsen.

Comments