MRISHO NGASA AONA MWEZI VPL LEO

MFUNGAJI bora wa ligi kuu soka Tamnzania Bara msimu uliopita, Mrisho Ngasa wa Azam Fc leo ameifungia timu yake ya Azam bao lake la kwanza kupitia mechi yao na JKT iliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Ngasa alifunga bao hilo katika sekunde ya 36 ya mchezo huo, hivyo kutoa doa la kutocheka na nyavu tangu kuanza kwa ligi hiyo Agosti 20 mwaka huu.

Katika mechi hiyo Azam ilishinda mabao 2-0, ambapo bao la pili lilipachikwa na John Bocco katika dakika za nyongeza na hivyo kuifanya Azam kufikisha pointi 18 na kushika nafasi ya tatu kwenye ligi hiyo.

Comments