MR.FLAVOR KUPAMBA FAINALI ZA BSS, MSHINDI KUONDOKA NA MIL.40

MSANII kutoka nchini Nigeria Chris Trent maarufu kama ‘Mr.Flavour ’ ambaye anatamba na singo ya yake ya ‘Ashawo’ anatarajiwa kutumbuiza katika fainali za shindano la vipaji la Bongo Star Search Second Chance linalotarajiwa kufanyika Oktoba 14 kwenye ukumbi wa Diamond Jubillee jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo, Ritha Poulsen alisema kuwa  msanii huyo pamoja na wengine kutoka hapa nchini watapamba fainali hizo zitakazoshirikisha wasanii watatu waliotinga fainali.
Alisema jumla ya shilingi mil.55 zitawaniwa katika shindani hilo ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi milo.40, mshindi wa pili atapata mil.10 na mshindi wa tatu atapata shilingi mili.5.

Comments