MR FLAVOR KUTUA KESHO TAYARI KUKAMUA FAINALI ZA BSS


MSANIII wa muziki kutoka nchini NIGERIA N’ABANIA maarufu kama MR FLAVOR anayetamba na kibao chake cha ASHAWOO katika vituo mbali mbali vya redio nchini atawasili KESHO nchini saaa tano usiku akitokea nchini NIGERIA tayari kwa kutoa burudani katika fainali za shindano la BONGO STARS SEARCH SECEOND CHANCE litakalofanyika tarehe 14 mwezi huuu katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE.


Mkurugenzi wa BENCHMARK PRODUCTIONS ambao ndio wa ratibu wa shindano hilo RITHA PAULSEN amesema maandalizi yamekamilika ya onyesho hilo ambapo wanatarajia msaniii huyo kuwasili usiku ambapo alhamisi atazungumza na wanahabari.

RITHA amesema kuwa washiriki wannne tu ndio watakaochuana vikali katika kumsaka mshindi wa shindano hilo atakayejinyakulia shilingi milioni 40, mshindi wa pili milioni 10 na mshindi wa tatu milioni 5.


Tiketi za onyesho hilo zimeanza tarehe ambapo zinapatikana katika vituo vya ,maduka ya SHEAR ILUUSION,BEUTY POINT,BIG RESPECT KARIAKOO,MANYWELE ENTERETIMENT,STEEERS na DIAMOND JUBILEE.


Amewataja washiriki hao ni pamoja na WAZIRI SALUMU MWENYE NAMBA BSS 23,ROGERS LUCAS BSS 27,BELA KOMBO BSS 05 na HAJI RAMADHANI BSS 11.

Comments