MISS MTWARA 2011 AFARIKI DUNIA

TASNIA ya urembo Tanzania imepata pigo baada ya mrembo wa mkoa wa Mtwara mwaka 2011 Rahma Swai kufariki dunia usiku wa kuamkia leo huko Mtwara.
Kwa mujibu wa mwandaaji wa shindano la Miss Mtwara, Rajab Mchatta, kifo cha marehemu kimetokana na ugonjwa wa  shinikizo la Damu.
Mchatta amesema mwili wa marehemu utasafirishwa kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam kwa Mazishi ambapo msiba upo nyumbani kwa bibi wa marehemu eneo la Changanyikeni.
INNA LILLAH WAINAILAIH RAJUN.

Comments