MAKOCHA 30 KUWANIA LESENI DARAJA C

Kozi ya ukocha kwa ajili ya kupata leseni za daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanzia Novemba 7 hadi 20 mwaka huu. Makocha 30 wameteuliwa na TFF kwa ajili ya kushiriki kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi wanne, mmoja wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), wawili wa CAF na mmoja wa Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU).
Mkufunzi wa FIFA atakuwa Jan Poulsen, kutoka CAF ni Sunday Kayuni (Tanzania), Kasimawo Laloko (Nigeria) wakati kutoka Denmark ni Kim Poulsen.
Makocha walioteuliwa kushiriki kozi hiyo ni Christopher Eliakim, Jumanne Ntambi, Keneth Mkapa, Mussa Furutuni, Mecky Maxime, Gideon Kolongo, Maka Mwalwisi, Haji Amir, Tiba Mlesa, Stephen Matata, Wane Mkisi, Edward Hiza, Leonard Jima na Ahmed Mumba.
Wengine ni Peter Mhina, Absolom Mwakyonde, Maarufu Yassin, Mussa Kamtande, Wilfred Kidau, Eliasa Thabit, Dismas Haonga, Fulgence Novatus, Juma Mgunda, Hassan Banyai, Mohamed Tajdin, Sebastian Nkoma, Emmanuel Massawe, Gabriel Gunda, Abdul Nyumba na Richard Kabudi.
Pia kutakuwa na kozi nyingine ya juu ya leseni za daraja B ambayo inatarajia kufanyika baadaye Desemba mwaka huu.

Comments