MAAFANDE WA OLJORO WAKALIA KITI CHA LIGI KUU BARA

MAAFANDE wa Oljoro JKT wameishusha kileleni vinara wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Simba, baada ya kuifunga Moro United ya Dar es Salaam kwa bao 1-0.

Mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid mjini Arusha ilikuwa na upinzani mkubwa kwani makosa waliyoyafanya mabeki wa Moro United katika dakika 34, yalimpa nafasi mshambuliaji wa Oljoro, Meck Michael, kucheka na nyavu za Moro.

Bao hilo lilisababisha timu zote kushambuliana kwa zamu huku pia zikiwa makini katika kulinda kuta zao ili kutotoa nafasi ya nyavu kutikiswa, hali iliyomaliza dakika 90 kwa Oljoro kuondoka kifua mbele kwa bao 1-0.

Kwa ushindi huo, sasa maafande hao wamefikisha pointi 19, hivyo kuongoza ligi hiyo baada ya kucheza mechi kumi, huku Simba waliokuwa vinara wakishuka hadi nafasi ya pili kutokana na kuwa na pointi 18 walizozipata kupitia mechi nane walizocheza, na nafasi ya tatu inashikiliwa na Azam FC yenye pointi 15.

Comments