'LUNDENGA AMZUIA MISS TANZANIA KUJIPONGEZA'

SHEREHE za kujipongeza kwa ushindi katika fainali za Miss Tanzania 2011 za warembo kutoka Kanda ya Ilala wakiongozwa Salha Israel zilizofanyika jana kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam ziliingia dosari baada ya mrembo huyo kutoonekana.

Katika sherehe hizo zilizohudhuria na wageni mbalimbali waalikwa, warembo wa Redds Miss Ilala waliong’ara katika fainali za Miss Tanzania na kuandaliwa sherehe hiyo mbali ya mshindi Salha, wengine Alexia William aliyeshika nafasi ya tatu na mshindi wa tano Jeniffer Kakolaki.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Redds Miss Ilala, Jackson Kalikumtima, mbali na kuelezea rekodi nzuri za warembo wa Miss Ilala katika mashindano ya Taifa, alisema, Salha ameshindwa kuhudhuria kutokana na mtu anayeitwa Hashim Lundenga, (Mratibu wa Miss Tanzania), kumzuia na kuwa ndiye anayejua sababu za kufanya hivyo.

“Nimeongea na Salha, kaniambia kuwa Lundenga kamzuia asihudhurie katika sherehe hii, sijui kwanini, lakini aelewe hadi anapatikana Salha sisi tumefanya kazi kubwa na bila sisi waandaaji wa kanda, mafanikio ya taifa ni ngumu kupatikana,” alisema Kalikumtima.

Naye mwakilishi wa JB Belmont, Mohamed Bawazir alisema, wamesikitishwa na uamuzi huo wa Lundenga, kwani wao wana historia ndefu na Miss Tanzania huyo hata kabla hajaanza kushiriki mashindano ya vitongoji.

“Salha ni balozi wetu muda mrefu, ambako amekuwa akilipwa na hoteli yetu mshahara, malazi na huduma mbalimbali, kwa hiyo tumekuwa tukifanya naye kazi muda mrefu na hapa ndipo alipotokea, sasa kwa kitendo hiki kwa kweli Lundenga ametusikitisha sana,” alisema Bawazir.

Akizungumzia hali hiyo, Lundenga alikiri kumzuia Salha kwa madai utaratibu uliotumika kumuomba haukufuata taratibu.
“Hivi sasa Salha yuko chini ya Kamati ya Miss Tanzania, hivyo mialiko yake lazima ijulikane na izingatie ‘interest’ za wadhamini wetu, sio aende kwenye shughuli halafua akatangaze bidhaa ya mtu mwingine,” alifafanua Lundenga.

Lundenga aliongeza kuwa, pia Kalikumtima aliwadharau sana kwa kuwapa taarifa za kumuomba Salha saa 10 jioni siku ya tukio.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHOctober 17, 2011 at 6:08 AM

    NO..HASHIM YUKO RIGHT KATIKA HILI,KINA JK NA HUYO JAMAA WA HOTEL WAMECHEMKA,HUYO MSICHANA SASA HIVI WAELEWE HATA KAMA ALITOKEA HUKO KITONGOJINI KWAO SIO WAO TENA,NI WA TAIFA HIVYO LAZIMA INTEREST ZA WADHAMINI WA KITAIFA ZIWE MBELE,WAO NDIO WANAINGIA GHARAMA KUBWA TOKA USIKU ULE ALIPOSHINDA HILO TAJI...JK RAFIKI YANGU NIMEFANYA NAE KAZI,HASHIM PIA RAFIKI YANGU NA PIA TUNAJUANA KI YANGA YANGA...LAKINI KWA HILI BWANA JK ACHA HASHIM AITWE HASHIM,SORRY

    ReplyDelete

Post a Comment