LIGI SOKA DARAJA LA KWANZA KUANZA KESHO

Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza hatua ya makundi msimu huu inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini inaanza Oktoba 15 mwaka huu. Jumla ya timu 18 zinashiriki katika ligi hiyo.

Kundi A kesho itakuwa Temeke United vs Polisi Dar es Salaam (Uwanja wa Mlandizi, Pwani) na Mgambo Shooting vs Transit Camp (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga). Mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Burkina na Morani itachezwa Oktoba 16 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mechi za kundi B kesho ni Polisi Iringa vs Small Kids (Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora, Iringa), Tanzania Prisons vs Mbeya City (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya) na Mlale JKT vs Majimaji (Uwanja wa Majimaji, Songea).

Kundi C kesho ni AFC vs Manyoni (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Polisi Morogoro vs 94 KJ (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Polisi Tabora vs Rhino (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).

Ligi hiyo itaendelea tena Oktoba 19 mwaka huu kwenye viwanja tofauti. Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 30 mwaka huu na kupisha dirisha dogo la usajili litakaloanza Novemba 1 hadi 30 mwaka huu. Mzunguko wa pili wa ligi hiyo utaanza Januari mwakani.

Comments