KUWAONA SIMBA, JKT RUVU 10,000

Viingilio katika mechi namba 66 kati ya Simba na Ruvu Shooting itakayochezwa kesho (Oktoba 19 mwaka huu) Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam ni sh. 10,000 kwa VIP n ash. 5,000 kwa mzunguko.


Tiketi za mechi hiyo zitauzwa uwanjani Chamazi katika magari maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo.

LIGI DARAJA LA KWANZA


Ligi Daraja la Kwanza hatua ya makundi inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini inaendelea tena kesho (Oktoba 19 mwaka huu) kwa mechi saba katika viwanja tofauti.
Katika kundi A, Polisi Dar es Salaam itacheza na Burkina Faso ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani wakati Transit Camp itakuwa mwenyeji wa Temeke United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Nayo Mgambo Shooting itakuwa mgeni wa Morani katika mechi itakayochezwa mkoani Manyara.
Kundi B itakuwa kati ya Small Kids na Tanzania Prisons zitakazocheza mjini Morogoro, Mbeya City itaumana na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine. Kundi C ni kati ya Manyoni FC na Polisi Morogoro itakayochezwa mjini Singida wakati Rhino FC itakuwa mwenyeji wa AFC kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mechi kati ya Majimaji na Polisi Iringa ya kundi A yenyewe itachezwa Oktoba 20 mwaka huu Uwanja wa Majimaji mjini Songea kama itakavyokuwa kwa mechi ya kundi C kati ya 94KJ na Polisi Tabora itakayochezwa Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.

Comments