KLABU LIGI KUU ZAZIDI KUIBANA PUMZI TFF

MSIGANO kati ya klabu za Ligi Kuu Bara na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuhusiana na usimamizi wa ligi umezidi baada ya klabu hizo kuunda kamati yao huku pia wakitishia kugoma endapo hawatalipwa madai yao yote.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ya klabu za Ligi Kuu katika uundwaji kwa kampuni ya usimamizi wa ligi hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu' alisema, wamekutana na kujadili mambo kadhaa na kwa pamoja wameamua kutoshiriki ligi hiyo endapo TFF watashindwa kuwalipa fedha zao zote wanazodai.
Kaburu alisema, maamuzi hayo yametokana na ukimya wa Shirikisho hilo na kushindwa kutoa fedha zinazotoka kwa wadhamini wakati unaotakiwa, kwani huzitumia na kujikuta wakishindwa kuzilipa klabu kwa wakati.

Pia alisema katika kikao hicho maalumu kilifanya uteuzi wa kamati ya klabu katika mchakato wa kuundwa kwa Kampuni ya Usimamizi wa Ligi Kuu Bara na Ligi Daraja la Kwanza.
Aliongeza kuwa hadi msimu wa ligi mwakani, kampuni itakuwa tayari imepatikana na kuendesha ligi ikiwa huru na si kusimamiwa na Kamati ya Mashindano kama ilivyo sasa.
Alisema wanatarajia kuwasilisha barua ya maamuzi yao TFF, kuwapa taarifa ya uundwaji wa kamati hiyo, pamoja na kulipwa fedha zao wanazodai.
Hivi karibuni pande hizo zimekuwa zikivutana katika uundwaji wa chombo cha kusimamia ligi, ambapo klabu zinataka kampuni huku TFF ikipigia chapuo kamati.

Comments

  1. YANGA BOMBA- UHURU BRANCHOctober 23, 2011 at 6:12 PM

    HAYO NDIO MAMBO TUNAYOPENDA KUSIKIA JAPO YAMECHELEWA SANA...DUNIANI KOTE FA HAISIMAMII LIGI BALI NI VILABU HUSIKA NDIO VYENYE JUKUMU HILO,FA WAO WANASAIDIA MASUALA YA KUFUNDI TU BASI LAKINI JINSI GANI LIGI IWE FEDHA ZA UDHAMINI MAPATO YA MILANGONI NA MAMBO KAMA HAYO YANYOVIHUSU VILABU MOJA KWA MOJA YANASIMAMIWA NA VILABU VYENYEWE THROUGH COMPANY,KENYA WALISHAANZA UGANDA NAO LAST YEAR NADHANI WALIANZA SASA HIVI WANA SEASON YA PILI NA MAMBO YANAKWENDA..ANAGALIZO SASA HAPO USIMBA NA UYANGA UWEKWE PEMBENI,TFF WAMEKUA WAKIUTUMIA HUO KUWAGAWA NA KUFANYA MIPANGO YA KUDAI HAKI KWA PAMOJA KUSHINDIKANA ILI WAO WAENDELEE KUVINYONYA VILABU,HIYO NI TYPICAL DIVIDE AND RULE SYSTEM,SIMBA NA YANGA AMKENI SASA

    MDAU YANGA BOMBA,GRAND RAPIDS,MICHIGAN,USA

    ReplyDelete

Post a Comment