KIBADENI AENDA KUTIMIZA IBADA YA HIJJA

ALIYEKUWA meneja wa timu ya soka ya Simba, Abdallah Kibadeni ‘King Mputa,’anatarajia kuondoka nchini kesho kwenda  Makka, Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Hijja.

Kibadeni amesema kuwa anamshukuru mungu kwa kuweza kutimiza ibada hiyo ambapo pia akiwa huko pia dua zake atazielekeza kwa Wekundu hao wa Msimbazi kwa kuwaombea watwae Ubingwa wa vLigi Kuu soka Tanzania Bara na michuano ya Shirikisho.

Comments