KAGO AREJEA MSIMBAZI

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba, Gervas Kago amerejea nchini akitokea kwao Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kago alikuwa kwao kuitumikia timu yake ya Taifa iliyokuwa ikicheza mechi yake ya kuwania kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwakani.
Msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kuwa tayari mchezaji huyo ameshajiunga na wenzake waliopo kambini kwenye hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Simba itashuka katika dimba la Taifa Oktoba 16 mwaka huu kukwaana na African Lyon katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania Bara.

Comments