KABURU KUONGOZA KAMATI YA KUUNDA KAMPUNI YA KUSIMAMIA LIGI KUU

KLABU 14 za Ligi Kuu Tanzania Bara zimemteua Makamu  Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' kuwa Mwenyekiti wa kamati maalum ambayo itasimamia mchakato wa kuunda kampuni itakayosimamia Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza.
Katika kikao cha wawakilishi wa vilabu kilichofanyika jijini Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa Yanga Mwesiga Celestine aliteuliwa kuwa  makamu wakena Katibu Mkuu wa kamati hiyo ni Majori Ruta kiongozi wa  Ruvu Shooting.


Wajumbe wa kamati hiyo ni Iddi Godigodi kutoka klabu ya Villa Squad, Evodius Mtawali kutoka klabu ya Simba, Said Mohamed na Shani kutoka Azam FC.
Kamati hiyo itasimamia mchakato wa kuundwa kampuni hiyo na kutoka katika Kamati ya Mashindano ya TFF.

Comments