IMANI LISU WA BSS KUTAMBULISHWA K-MONDO SOUND J'MOSI

BENDI ya muziki wa dansi ya K-Mondo Sound jumamosi inatarajiwa kuwatambulisha wasanii wake wapya Iman Lissu na Salum Kumpeneka ‘Dk.Kumpeneka’, kupitia onyesho lake litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Zhong Hua Garden, Uliopo Morocco jijini Dar es Salaam.

Mwimbaji na Kiongozi wa bendi hiyo, Richard Mangustino, alisema jana kwamba watawatambulisha rasmi wasanii hao weapya ambao wamejiungana na bendi hiyo hivi karibuni.

Alisema, wamemnyakua Lisu ambaye alitolewa katika shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS), pamoja na Dk. Kumpeneka aliyewahi kutamba na kibao chake cha Dk. Ili kuongeza nguvu katika safu ya uimbaji wa bendi hiyo.
Mbali na onyesho hilo, K-Mondo ambayo kila Ijumaa hupiga katika Ukumbi wa Triz Motel.

Comments