HATMA YA MICHAEL WAMBURA KUGOMBEA UENYEKITI FAM KUJULIKANA KESHO

HATIMA ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Tanzania (FAT sasa TFF), Michael Wambura, kuwania nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM), inatarajiwa kujulikana kesho baada ya kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo.

Wambura aliwekewa pingamizi la kuwania nafasi hiyo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Tito Osoro kwa madai kwamba Wambura si mkazi wa Mara na aliwahi kupeleka masuala ya soka mahakamani.
Osoro pia amesema Kamati ya Rufaa ya TFF ilishawahi kueleza kuwa, Wambura si muadilifu,kwani  aliondolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa Shirikisho hilo 2008.Uchaguzi wa FAM umepangwa kufanyika Novemba 13 mwaka huu katika Wilaya ya Rorya mkoani Mara.
Kwa upande wake, Wambura ameitaka kamati hiyo kumtendea haki kwa kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi, kwani imezoeleka kuwa, kila anapojitokeza kuwania nafasi ya uongozi kuwekewa mizengwe.

Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHOctober 23, 2011 at 6:23 PM

    MICHAEL MBONA ILISHAELEZWA NA KUTHITISHWA NA KAMATI YA UCHAGUZI KWAMBA ANAKOSA SIFA MOJA MUHIMU SANA "UADILIFU" ,NA MIMI NINAVYOJUA UADILIFU HAUSOMEWI POPOTE NI KITU CHA KUZALIWA NACHO SASA MICHAEL NDUGU YANGU UADILIFU WA GHAFLA NAMNA HII UMEUPATA WAPI?ACHA KUPENDA MADARAKA KIASI HICHO,WALIPOSEMA HUNA DEGREE UKAAMUA KUSOMA MPAKA MASTERZ KUWAKOMESHA LAKINI UADILIFU SASA KAKA NDIO TATIZO!

    MDAU WA BOMBA, USA

    ReplyDelete
  2. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHOctober 23, 2011 at 6:24 PM

    HALAFU ULIONA WAPI MTU ULISHAKUA KATIBU MKUU WA TFF TAIFA LEO UKAGOMBEE UENYEKITI WA MKOA?!!!MBONA WABONGO MNAPENDA SANA UKUBWA KIASI HIKI?

    ReplyDelete

Post a Comment