FELLA AFUNGUKA KUHUSU SONGI LA KUSONONASONONA'

KIONGOZI wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Fella ‘Mkubwa Fella’, amesema singo yake inayokwenda kwa jina la ‘Kusononasonona’ imelenga kuwaonya Mama na mawifi.
Fella alisema kuwa wimbo huo haumlengi mtu, lakini unazungumzia matukio yanayojitokeza kila kukicha katika jamii ambapo akina mama wengi huwashawishi watoto wao wa kiume kuwaoa wasichana wanaowataka wao, lakini baada ya ndoa hubadilika na kuanza kuwachukia wake hao.
“Mkubwa maana na wimbo huu wa ‘Kusononasonona’ ni wimbo wa kuwakacha mama na mawifi kwamba wauache mke ambaye awali walikuwa wakimpenda lakini alipoolewa wakamgeuka na kuanza kumchukia,” alisema Fella.
Fella aliongeza kuwa watu wa ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kuanzia Lamu na Mombasa Kenya, pamoja na Tanga, Bagamoyo, Zanzibar, Dar es Salaam, Mafia, Lindi na Mtwara wanaifahamu vema lugha hiyo na tabia za Mama mkwe na Mawifi.

Comments