COSTA, KADO WAACHWA STARS, CANAVARO APOZWA KWA UNAHODHA

BEKI wa kutumainiwa Taifa Stars ikiondoka jioni ya leo kuelekekea katika jiji la Cassablanca nchini Morocco,beki wa timu hiyo Victor Costa na kipa Shaban Kado wameachwa kwenye kikosi hicho, huku mshambuaji wake Mrisho Ngasa akibeba mizigo ya unahodha.

Kikosi cha wachezaji 20 kimeondoka kikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vema katika mechi yake ya mwisho ya mchujo kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani katika nchi za Equatorial Guinea na Gabon itachezwa Oktoba 9 mwaka huu katika jiji la Marrakech nchini humo.
Ofisa habari wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema kuwa Costa ameachwa kutokana na kuwa majeruhi,akiungana na majeruhi wengine katika timu hiyo ambao pia wameachwa, Shadrack Nsajigwa na Amir Maftah.
Alisema kuwa timu hiyo ilikabidhiwa bendera juzi usiku katika hafla maalum waliyoandaliwa wachezaji wa timu hiyo ambapo wameahidi kucheza kufa na kupona kuhakikisha wanashinda mechi hiyo ya kundi D.
“Pamoja na kuwa nafasi ya Stars ni finyu kufuzu kucheza fainali hizo lakini watahakikisha wanacheza na kushinda na hata kama wasipofuzu watajiwekea heshima,”Alisema.
Aliwataja wachezaji walioondoka kuwa ni pamoja na Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), na Juma Kaseja (Simba).Mabeki wa pembeni ni nahodha Nadir Haroub 'Canavaro' (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) wakati mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam).
Viungo wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar) na Jabir Aziz (Azam). Viungo washambuliaji ni Mrisho Ngassa (Azam) na Ramadhan Chombo (Azam). Washambuliaji ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), John Bocco (Azam).
Mbali na mechi hiyo itakayopigwa saa 1.30 usiku siku hiyo na wakati huo pia itachezwa mechi nyingine ya kundi hilo itakayozikutanisha Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati utakaochezwa Algiers, Algeria ambapo lengo ni kuepuka kupanga matokeo. Mechi hiyo itachezwa jijini Algiers.
Waamuzi wa mechi kati ya Stars na Morocco watakuwa Gassama Bakary, Jawo Dickory, Touray Sulayman na Camara Bakary, wote kutoka Gambia. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Zoumaro Gnofame kutoka Togo.

Comments