CHIPUKIZI AFRICAN LYON WAULA MAREKANI

WACHEZAJI watano wa timu ya vijana chini ya miaka 20 ya African Lyon wanatarajia kwenda nchini Marekani  kucheza soka la kulipwa katika  vituo vya kuibua vipaji vya soka nchini humo.

 Mkurugenzi wa timu hiyo, Rahim Zamunda alisema mchezaji Hamis Thabit ambaye ni mmoja wa wachezaji hao anatarajia kuondoka nchini kesho akielekea kwenye kituo cha soka cha Seatle Sounders ambako atalelewa katika kitup hicho kwa miaka mitatu.
Zamunda alisema nyota mwingine aliyepata ofa hiyo ni Jarufu Kizombi ambaye aliibuliwa na mpango wa Serengeti Soccer Fiesta ambaye anatarajia kupelekwa katika kituo cha Louisiana cha Marekani kwa miaka minne yeye  anatarajia kuondoka mwezi ujao.
"Pia wachezaji Abdu Seif, Razak Khalfan na Hood Mayanja ambao wanakwenda huko  na kisha watatafutiwa timu za kucheza,"Alisema.

Comments