BEKI wa kushoto wa Yanga, Stephano Mwasika ambaye alikuwa akiandamwa na majeruhi ya goti kwa muda mrefu, ameanza mazoezi na wenzake baada ya hali yake kutengemaa.
Mwasika aliumia wakati timu yake ilipocheza mechi ya kwanza ya ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya African Lyon kabla ya kujitonesha katika mazoezi ya Timu ya Taifa 'Taifa Stars' hivyo kulazimika kukaa nje kwa miezi mitatu.

Comments