AZAM YAZISHUSHA YANGA, OLJORO

Timu ya soka ya Azam leo imefanikiwa kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kuifunga Polisi Dodoma kwa mabao 3-1.
Kwa ushindi huo Azam imefikisha pointi 21 hivyo kuzishusha Oljoro JKT iliyokuwa ya pili kwa kuwa napointi 19 na Yanga iliyokuwa ya tatu kwa pointi 18.
Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 24.

Comments