AZAM FC YAISHUSHA YANGA, YATIBUA REKODI ZA JKT RUVU

USHINDI wa mabao 2-0 iliyoupata Azam Fc leo katika mechi yake na JKT Ruvu umepelekea kuwashusha nafasi moja mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga.
Yanga ambayo ilikuwa inashika nafasi ya tatu kwenye ligi hiyo sasa imeshuka hadi nafasi ya nne kutokana na pointi 15 ilizonazo huku Azam ikipanda katika nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 18.
Kwa mantiki hiyo JKT Oljoro wanaewndelea kukalia kiti cha ligi hiyo wakiwa na pointi 19, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Simba yenye pointi 18.

Comments