YANGA YAONA MWEZI CHAMAZI

MABINGWA watetezi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga leo wamepata ushindi wao wa kwanza katika ligi hiyo baada ya kuifunga African Lyon kwa mabao 2 – 1, katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Azam uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yalifungwa na Davis Mwape katika dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza na Rashid Gumbo dakika ya 66 ya kipindi cha pili, huku Lyon wakijipatia la kufutia machozi kupitia kwa Shengo aliyefunga kwa mpira uliokufa (freekick) dakika ya 44 kipindi cha kwanza. Mabingwa hao watetezi wa Ligi sasa wamefikisha pointi 6 katika michezo 5 iliyokwishacheza.

Comments

  1. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHSeptember 15, 2011 at 10:43 PM

    PISHA NJIA TUNAKUJA...TUMEANZA LIGI RASMI SASA,SISI KWISHAJUA JANJA YA WANYAMA SASA,YALE MAJINA YA WACHEZAJI WETU YALIYOKUWA YAMEZIKWA KABURINI PAMOJA NA MAITI NA WAPINZANI WETU TUMESHAYAFUKUA WAAMBIE...SASA TUCHEZE MPIRA UWANJANI TUONE NANI ZAIDI..WANYAMA WANA KUFURU MBAYA SANA AISE,YANI WANAZIKA MAJINA YA WATU WALIO HAI,HII NI DHAMBI HATA KWA SHETANI,SASA MTATUKOMA!

    MDAU WA BOMBA,GRAND RAPIDS,MICHIGAN,USA

    ReplyDelete

Post a Comment