YANGA, LYON WAINGIZA MIL.14 CHAMAZI



Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya African Lyon na Yanga iliyochezwa Septemba 15 mwaka huu Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam imeingiza sh. 14,929,000.
Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 2,038 ambapo kiingilio kilikuwa sh, 7,000 kwa mzunguko na sh. 20,000 kwa VIP. Waliokata tiketi za sh. 20,000 walikuwa 51.
 
Baada ya kuondoa gharama za mchezo ambazo ni sh. 3,123,409.49 na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 2,277,305.08 kila timu ilipata sh. 3,182,888.47.
Mgawo mwingine ulikwenda kwa uwanja (sh. 1,013,409.49), TFF (sh. 1,013,409.49), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 506,704.75), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 527,643.80) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 101,340.95).

Comments