WANACHAMA YANGA WAMSHUKIA NCHUNGA, WASEFA TIMU INAFANYA VIBAYA VPL SABABU YAKE

WANACHAMA wa tawi la Yanga Umoja lenye maskani yake Tandale jijini Dar es salaam wamemtaka Mwenyekiti wa klabu hiyo Taifa Loyd Nchunga kuacha chuki zake binafsi zinazosababisha kuchonganisha Wanayanga na hatimaye timu kufanya vibaya katika ligi kuu inayoendelea hivi sasa.
Wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa tawi hilo Juma Miraji walisema kuwa Nchunga amekuwa akilichukia tawi hilo kutokana na maovu yake baada ya uongozi wao kukataa rushwa kadhaa alizozitoa ili achaguliwe kuwa Mwenyekiti.
“Sisi leo tumeamua tuseme kuwa Wanayanga wasishangae kwa nini Yanga inafungwa ni kutokana na Nchunga kuanzisha migogoro yake binafsi baada ya kutaka tawi letu lifutwe uanachama na sisi kamwe hatutakaa kimya bali tutasema ana maovu mengi na maovu hayo ndiyo matokeo ya timu kufungwa”alisema Said Bakari Msemaji wa Tawi.
Saidi alisema tangu Nchunga aingie madarakani kumekuwa na matatizo mengi yakiwemo ya kuvunjwa kwa katiba na kufanya mambo yake binafsi hali inayosababisha migogoro sanjali na kutolipa Wachezaji posho zao.
Alisema kuwa Nchunga amekuwa akisababisha kutoelewana baina yao baada ya kukataa kumuunga mkono na hivyo kujenga chuki na tawi hilo hali iliyopelekea kufanya ushawishi katika kamati tendaji ili wafutwe uanachama ikiwa ni moja ya ajenda za mkutano mkuu ujao.
Walisema hawatakubali kuvuliwa uanachama kiholela kwa kuwa wao ni wanachama halali wa Yanga tangu mwaka 2008 na kuwa hawawaungi mkono wazee hao wanaodai katiba ya mwaka 1968 ili kuwaondoa madarakani.
“Sisi hatushangai kufungwa kwa Yanga tunajua ni madhambi ya Nchunga kwa kuwa hakutaka kulipisha hili hadi ligi iishee ndipo aanzishe mgogoro huu na sisi hatungoji ligi iishee tunamjibu kuwa akitufuta uanachama tunasubiri uongozi mwingine tunaomba tena na tutapata hatua makosa sisi”aliongeza Mwenyekiti msaidizi Juma Miraji.
Juma alisema kuwa Nchunga amekuwa akijichukulia maamuzi yake binafsi bila kushauriana na wenzake zaidi mtu aliyekuwa naye karibu hali inayosababisha timu hiyo kufanya vibaya katika ligi inayoendelea sasa.
Juma alisema kuwa kutokana na madhambi hayo ya uonevu,chuki na kutofuata ushauri wa wenzake kutaendelea kuifanya Yanga kufungwa mara kwa mara hadi hapo Nchunga atakaoondoka madarakani na kupisha uongozi mwingine wenye uzalendo ndipo Yanga itarudi katika hali nzuri ya ushindi.
Aidha kwa niaba ya Wanachama waliokuja katika ukumbi wa habari maelezo Msema ji wa tawi hilo alisema kuwa Wapenzi wa timu ya Yanga wasishangae kwani Yanga inafungwa ni kutokana na Nchunga kutofuata mikataba ya Wachezaji na kuendekeza migomo ambayo haina tija kwa klabu.

Comments

  1. HAO WANACHAMA WAAMBIE TIMU INAFANYA VIBAYA KWA AJILI YAO SI NCHUNGA,HILO TAWI LA TANDALE SIKU ZOTE NI PROBLEM,MBONA YANGA ILPOTWAA UCHAMPION WA AFRICA MASHARIKI NA KATI HAWAKUSEMA NI KWA AJILI YA NCHUNGA?WAO TANDALE WALICHANGIA NINI KUISAIDIA YANGA KUTWAA UBINGWA WA BARA,TUSKER NA AFRICA MASHARIKI,WAAMBIE KINA MATANDIKA WAACHE MAJUNGU,MIMI BAHATI MBAYA NI MAREKANI KWA SASA LAKINI WANANGU PALE UHURU WANANIPA INFO KILA SIKU ZA KINACHOENDELEA,TOKA ENZI ZA TARIMBA TANDALE NI SHIDA TU,BORA LIFUTWE,KUNA DOGO PALE ANAITWA JITU TULIKUA NAE BOMBA UHURU ZAMANI AKAJITOA,YEYE NA HUYO SAID SASA NDIO WANALIENDESHA HILO TAWI KWA MASLAHI YAO.

    ReplyDelete
  2. YANGA BOMBA -UHURU BRANCHSeptember 9, 2011 at 5:04 PM

    HALAFU WE MNYAMA UNAJUA SIE WENGINE TUKO MBALI NA TANZANIA SO TUNAKUTEGEMEA WEWE KWA HABARI HIZI ZA VILABU VYETU VIKONGWE NA KINACHOENDELEA KIUJUMLA KWENYE VPL NA SOKA LA BONGO KIUJUMLA,HII HABARI MBONA UMEIWEKW KATIKA ANGLE TOFAUTI NA ILIVYO?WANANGU WA BOMBA UHURU NIMEWASILIANA NAO WAMENIAMBIA KUMBE KILICHOTOKEA NA TFF KUIAGIZA YANGA IWAFUTIE UANACHMA WANACHAMA WAKE WALIOPELEKA MASUALA YA MPIRA MAHAKAMANI,KUMBE ISSUE SIO NCHUNGA KUWAANDAMA HAO WANACHAMA BALI ISSUE NI KUKIUKWA KWA MAELEKEZO YA TTF NA FIFA KIUJUMLA KUTOPELEKA MASUALA YA MPIRA MAHAKAMANI.HAO JAMAA WA TANDALE KINA JITU NA SAID WANAWEWESEKA TU.

    MDAU YANGA BOMBA-USA

    ReplyDelete

Post a Comment