YANGA WAPANIA KUREJESHA HESHIMA KWA COASTAL UNION KESHO

WAKATI kesho mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Yanga, wanatarajiwa kucheza na Coastal Union ya Tanga katika Uwanja wa Taifa, bara, wachezaji wa timu hiyo wameahidi ‘kuwafanyia kitu mbaya’ Wagosi hao wa Kaya.

Wakizungumza na gazeti hili jana kwa masharti ya kutotajwa majina yao, wachezaji hao walisema wanataka kurudisha heshima yao baada ya kuanza kwa kusua sua kwenye ligi hiyo.
Walisema, mwenendo wao wa kusuasua kwenye ligi hiyo umewashushia heshima mbele ya mashabiki wao na kuonekana kwamba hawajui soka wakati timu yao imesheheni wataalamu.
“Wengune wanatufanisha sisi na Arsenal wakati kiukweli ni bora kama Manchester United ila tu upepo ulikuwa mbaya hapa katikati”, Alisema mmoja ya wachezaji hao.
Alisema licha ya kuanza vibaya kwenye ligi hiyo, bado wanaimani ya kutetea tena ubingwa wao katika ligi ya mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka jana.
“Mwaka jana kuna mtu ambaye alijua kama tutatwaa ubingwa, sasa na mwaka huu tutawashangaza wengi kwani sisi kama wachezaji tunajua nini tunachofanya, hii ni sehemu ya mchezo hivyo sasa tumejipanga kurejesha heshima,”Aliingeza.
Yanga inayonolewa na Mganda Sam Timbe, inaendelea na mazoezi yake katika uwanja wake wa Kaunda, jijini Dar es Salaam, wakati Coastal wameapa kutokuwa uchochoro wa mabao kwa Wanajangwani.

Comments