WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO KAZI KWETU!

Katika nia nzuri ya kuongeza mvuto na kuwapatia habari wadau wa kandanda Tanzania na Duniani kwa ujumla, tovuti ya kandanda imefungua milango kwa wadau wanaoweza kuleta habari, makala au uchambuzi wowote.
Kwa utaratibu, kila kitu kitakachopokelewa katika dawati la tovuti ya kandanda kitanakshiwa ili kuwapa hamu na radha wasomaji kusoma zaidi na zaidi.
Mwandishi anaweza kuwa na makala ambazo ataleta kila baada ya muda wa makubariano  na tovuti, Makala hizo zitapewa majina kulingana na ujumbe utakaokuwa ukibebwa, vichwa vya vijisehemu viwe na mvuto kwa msomaji.
Kwa waandishi watakao tengeneza makala nzuri za kuvutia ndani ya Mwezi mmoja, watalipwa na tovuti kutokana na makala iliyotoka katika tovuti. Bei itakuwa ni makubariano ya tovuti (chini ya GALACHA design) na mwandishi husika. Hii itakuwa ni kama majaribio ya kujitolea kwa waandishi hawa ndani ya mwezi mmoja kuanzia Octoba mosi mpaka Octoba 31, 2011.
Lengo likiwa ni kuifanya tovuti ya kandanda sehemu ya habari za uhakika na zakichambuzi zaidi kutoka kwa wadau na wanamichezo wote.

Comments