VODACOM YASALIMU AMRI KWA YANGA

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania, imekubali kutoa nembo maalum kwa ajili ya klabu ya Yanga, ambayo itakuwa na rangi nyeusi, baada ya klabu hiyo kuikataa nembo mpya ya awali ya klabu hiyo, iliyokuwa na rangi nyekundu. 

Yanga iliikataa nembo hiyo kwa sababu utamaduni wake ni kuvaa rangi za kijani, njano na nyeusi, wakati rangi nyekundu ni alama kuu ya wapinzani wao wa jadi Simba. Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu amesema leo sasa mgogoro wao na wadhamini hao wa Ligi Kuu ya Bara umeisha na watapewa nembo mpya zenye isiyo haramu kwao.

Comments