VIONGOZI YANGA YANGA WASALIMU AMRI

UONGOZI wa klabu ya soka ya Yanga umeamua kusalimu amri ya Mahakamya ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyowazuia kufanya mkutano wake mkuu uliokuwa ufanyika kesho kwenye bwalo la Maofisa wa Polisi Oyesterbay.Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu alisema kwamba walipatiwa barua rasmi ya kuzuiwa kwa mkutano huo kutoka kwa mmoja ya wajumbe wa kamati iliyofungua kesi kupinga kufanyika kwa mkutano huo.
“Leo mchana tulipata rasmi barua kutoka Mahakamani ikieleza kuzuia mkutano huo, hivyo hatuna budi kuheshimu maamuzi yaliyotolewa na chombo hicho kikuu,”Alisema Sendeu.
Sendeu aliongeza kuwa, kutokana na kutofanyika kwa mkutano huo amewaomba radhi wanachama wote wa Yanga ambao walikuwa wamejiandaa kushiriki na kuwaomba kuwa watulivu mpaka maamuzi mengine yatakapotolewa.
Hatua hiyo inafuatia baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kufungua kesi ya msingi namba 98 ya mwaka 2010 ambayo iliisha kwa kuubatilisha uongozi wa klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake Lloyd Nchunga kutokana na kuwekwa na katiba batili.
Katika kesi hiyo ambayo hukumu yake ilitoka Julai 1, 2010 na kusisitizwa Agosti 29, mwaka huu, walalamikaji walikuwa wakipinga uhalali wa katiba ya sasa kwa hoja kuwa, katiba halali ni ya mwaka 1968 iliyosajiliwa kwa Kabidhi Wasihi.
Licha ya kubatilishwa kwa uongozi wa Nchunga, hivyo kutakiwa kuondoka madarakani kuipisha Kamati ya Muda chini ya Salim Gereza, bado yupo madarakani waliitisha iliitisha Mkutano Mkuu wa Mwaka.
Kabla ya kuzuiwa kwa mkutano huo, uongozi ulisema ungejadili ajenda mbalimbali zikiwemo kuwasilisha kwa wanachama mapato na matumizi ya klabu hiyo, kuwathibitisha wajumbe wa baraza la wadhamini na kuthibitisha kamati ndogo ndogo ambazo ziliteuliwa na uongozi mpya ulioingia madarakani Julai mwaka jana.
Aidha, mkutano huo pia ungewajadili wanachama waliofungua kesi ambao walisimamishwa na uanachama na kamati ya utenjdaji ya klabu hiyo wiki iliyopita.

Comments