TI ATOKA NA KUREJEA JELA

BAADA ya kuachiwa kutoka katika kuta za jela mapema wiki hii, alikokuwa akitumikia kifungo cha miezi 10 kutokana na dawa za kulevya, rapa T.1. amejikuta akirejeshwa tena lupango juzi usiku. Kilichomponza rapa huyo, ni kitendo chake cha kuamua kutumia basi la kifahari kwa ajili ya ziara ya kwenda nyumbani kwake maeneo ya Atlanta. T.I. aliachiwa kutoka katika kuta za jela, lakini ilikuwa kwa msamaha maalumu wa kumalizia siku zake zilizobaki nje ya gereza, lakini aliwekewa masharti kadhaa ambayo ameyakiuka.
Rapa huyo alinaswa na kamera akiwa katika basi hilo, ambapo ilidaiwa alitaka kuwepo maeneo hayo na kurejea haraka ili asifumwe na maafisa wa magereza.
Kwa mujibu wa maafisa magereza, rapa huyo alikuwa hatakiwi kusafiri kwa usafiri wowote ule kwenda nyumbani kwake bila kusindikizwa na askari na pia alitakiwa aseme ni usafiri gani atakaoutumia.
Wakili wa T.I., Steve Sadow alidai kulikuwa na mkanganyiko mkubwa lakini anaamini rapa huyo hakufanya jambo hilo kwa makusudi.

Comments