TFF YAKERWA NA MBWA WA BOBAN

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko tukio la mbwa wa polisi kukata kamba na kusababisha mtafaruku kwa wachezaji wakati wa mechi kati ya Toto Africans na Simba iliyochezwa Septemba 21 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba.

Tunafanya mawasiliano na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza ili kujua chanzo cha tukio hilo, na hatua ambazo jeshi hilo limechukua kwa mhusika iwapo itathibitika kuwa kitendo hicho kilisababishwa na uzembe.


Pia tunaamini kuwa tukio hilo litakuwa ni fundisho kwa askari polisi ambao badala ya kufanya shughuli iliyowapeleka uwanjani ya kulinda usalama ugeuka kuwa watazamaji wa mpira.

Comments