TFF WAANZA KUIBOMOA BOMOA RATIBA LIGI KUU

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko madogo ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid ulioko mkoani Arusha kuwa na shughuli nyingine za kijamii. Kati ya Septemba 7 na 8 mwaka huu, na Septemba 17 na 18 mwaka huu, uwanja huo utatumika kwa shughuli za dini na mashindano ya riadha ya Safari International Marathon.  Mabadiliko ya ratiba yanahusisha mechi zifuatazo na tarehe mpya zikiwa katika mabano; Septemba 7 mwaka huu mechi namba 20- Oljoro JKT vs Azam (Septemba 9), Septemba 10 mwaka huu mechi namba 22- Azam vs Simba (Septemba 11), Septemba 11 mwaka huu mechi namba 26- Ruvu Shooting vs Yanga (Septemba 10).
Septemba 17 mwaka huu mechi namba 38- Oljoro JKT vs African Lyon (Septemba 19), Septemba 21 mwaka huu mechi namba 43- Kagera Sugar vs Oljoro JKT (Septemba 22), Septemba 21 mwaka huu mechi namba 49- Ruvu Shooting vs African Lyon (Septemba 20) na Septemba 24 mwaka huu mechi namba 54- Toto Africans vs Oljoro JKT (Septemba 25).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Comments