SOPHIA KUFUNGUA MAONYESHO YA TWENDE


Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, Muheshmiwa Bi Sophia Simba,ndiye atafungua rasmi TWENDE
Semina za TWENDE,zinatoa mahali pa kuwasiliana na kuendelea katia biashara
Mategemeo ya kupata maudhurio makubwa,Kiingilio ni bure kwa kila mtu Kwa mwaka wa pili TWENDE, itafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Hafla hii ya jumuia itakayokua ikifunguliwa kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni kwa siku tatu mfululizo 15-17 Septemba 2011.
Kiingilio TWENDE ni bure kwa watu wote, ili kuweza kusababisha jamii ijihusishe kikamilifu na wanawake wajasiriamali na ndivyo hivyo kwa wanawake wajasiriamali kupata nafasi ya kuonyesha bidhaa na huduma zao ili kuweza kuwa na mawasiliano na kuendelea katika biashara Tanzania.
Meneja Mradi wa TWENDE,”Gloria Mongella alisema,Tunategemea maudhurio makubwa kwa wanawake zaidi mwaka huu, kwakua kiingilio ni bure na pia kwa sababu viwanja vya Mnazi Mmoja vipo katikati ya mji na kusababisha iwe rahisi kwa watu wengi kuudhuria” .
TWENDE itafunguliwa rasmi Alhamisi ya tarehe 15 Septemba 2011 Saa 5:00 asubuhi, na Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto ,Muheshimiwa Sophia Simba.
Bi Mongella aliongeza “Tunajisikia faraja kubwa kwa hafla hii ya TWENDE kufunguliwa na Waziri ,kwahivyo tunawahamasisha wanawake wote kuweza kuudhuria kwa wingi katika ufunguzi wa maonyesho ya TWENDE, na kutumia nafasi hii katika kukutana na wanawake mbali mbali wajasiriamali”.
TWENDE itakua na semina ya siku tatu ikidhamiria kuhamasisha ,kuelimisha na kuendeleza wanawake katika sekta mbalimbali ikiwemo,afya,sheria,biashara,na risala za kuhamasisha
“Elimu ni uti wa mgongo katika jamii yetu, kwahivyo tunawaamasisha watu wafike kwa wingi katika semina za TWENDE,ili waweze kupata ufahamu kutoka kwa watu mbali mbali waliobobea katika sekta ya biashara kama njia ya kujifunza mbinu katika biashara na kufanya wanawake wawe bora katika ujasiriamali Tanzania” alisema Hamis k.Omary,Meneja Masoko wa TWENDE.
Dhamira ya TWENDE,ni kutangaza nafasi ya mwanamke katika maendeleo kitaifa kwa kutambua umuhimu na mafanikio ya wanawake wajasiriamali wakiwemo na wale walemavu katika kuwatengenezea ajira, kuwatambulisha wanawake wajasiriamali kama mifano ya kuigwa,kusambaza taarifa za wanaofanya vizuri katika biashara,kuwa na muungano wa wanawake wafanyabiashara (TWENDE SACCOS), na kuwasaidia katika afya zao ,kujitegemea wenyewe, na kujitegemea kiuchumi.
TWENDE imedhaminiwa na Ubarozi wa Marekani wa Tanzania , Daily News, Habari Leo, Delfina, Perfect Machinery, Ultimate Security, Global outdoor systems, Dar life, Clouds FM, Vayle springs, Eventlites, Coca-Cola na 361 Degrees.

Comments