SIMBA, YANGA NA AZAM ZACHONGEA WAAMUZI TFF

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limepokea malalamiko ya waamuzi kutoka klabu za Simba, Yanga na Azam zilizochezwa hivi karibuni kwenye viwanja tofauti.
  Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema Azam waliwasilisha malalamiko ya mwamuzi wa mchezo dhidi yao na Ruvu Shooting uliochezwaSeptemba 26, Mlandizi Pwani hakuwa makini na mchezo huo. 
Wambura alisema malalamiko ya Simba yaliwasilishwa TFF ni ya mchezo dhidi ya Toto Africa uliochezwa wiki iliyopita kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wachezaji wa Simba walichezewa rafu za makusudi. 
Aidha Wambura alisema walipokea pia malalamiko ya mchezo kati ya Yanga na Ruvu Shooting mwamuzi wa mchezo huo kwamba aliipendelea Shooting.

Comments