SIMBA, YANGA MMEJIFUNZA NINI KUTOKA KWA AZAM FC!



Napenda niwaulize wadau kama kweli ni haki kwa Timu za Simba na Yanga kuufanya uwanja wa Azam FC kuwa kama uwanja wao wa nyumbani!! La hasha, kwa mimi nitasema si haki, ni kitendo cha aibu sana kwa timu hizi mbili kubwa ambazo kama tunavyoona hapo kwenye Logo zao zinaonyesha ni jinsi gani zilivyo vilabu kongwe hapa nchini lakini havina viwanja vyao vya kuweza kucheza mechi zao za ligi za nyumbani na za kimataifa.

KAPINGAZ Blog inawaomba Viongozi wa timu hizi mbili mlio madarakani kwa sasa muone hili ni kama changamoto kwenu kwa timu changa imeweza kuwa na uwanja wake, na timu zenu zikajikuta mnaenda kucheza kwenye uwanja huo, ni fedheha sana kwenu.
"USHAURI WA BURE VIONGOZI JITAHIDINI KUJALI MASLAHI YA TIMU"
Na Mdau, Henry Henry

Comments

  1. BORA HATA SISI ANGALAU TUNAO HATA WA MAZOEZI KULIKO WANYAMA NA ILE TAMTHILIA YAO ISIYOISHA YA KUJENGA UWANJA WA KISASA BUNJU...ALIANZA KADUGUDA NA TAMTHILIA HIYO ADEN AKAENDA NAYO MBALI ZAIDI KWA KUMLETA YULE MUARABU WA ARUSHA AKIDAI NI MTAALUM KUTOKA UTURUKI ALIYEKUJA KUFANYA TATHMINI YA JINSI GANI UWANJA MPYA WA KISASA UTAKAVYOKUA KUWA...KUJA KUCHUNGUZA KUMBE HATA HICHO KIWANJA HUKO BUNJU HAWANA...SISI WASANII LAKINI WANYAMA WENZETU WAMEZIDI KWA USANII..NASIKIA ADEN AKAWAONYESHA WANASIMBA MPAKA PICHA ZA JINSI UWANJA WAO WA KISASA UTAKAVYOKUA BAADA YA KUKAMILIKA ETI UTAKUA NA MADUKA SIJUI NA NINI...ADEN BWANA!

    LAKINI YOTE KWA YOTE TUACHE UTANI AZAM WAMETUVUA NGUO SIMBA NA YANGA,NAMKUMBUKA SANA MAREHEMU SYLERSAID MZIRAY ALIKUA AKIPINGA SANA KUZIITA SIMBA NA YANGA ETI NI TIMU KUBWA,YEYE ALIKUA AKISEMA SIMBA NA YANGA NI CLUB KONGWE TU HAZINA UKUBWA WOWOTE,INAWEZEKANA ALIKUA RIGHT KIASI FULANI.
    R.I.P.BROTHER

    ReplyDelete

Post a Comment